SALIM WILLIS MWANAMUZIKI ALIYETOKEA BENDI YA SHULE.
Shule nyingi sana za sekondari, katika miaka ya 70 na kurudi nyuma, zilikuwa na bendi za muziki wa magitaa. Wengi wa wanafunzi hawa hawakuendelea na kupiga muziki ukubwani, lakini wengine hawakuacha talanta hiyo na maisha yao yakaja kutegemea muziki.Salim Willis ni mmoja kati ya wanamuziki wa bendi za shule aliyefikia kuwa mwanamuziki wa bendi kubwa…
