DANSI LIMEBADILIKA SANA
Kumbukumbu zangu huwa zinanirudisha Iringa nilipokuwa na umri wa miaka minne hivi. Nadhani ndipo nilipoanza kutambua kuwa wazazi wangu walikuwa wanajitayarisha kwenda dansini, nakumbuka sauti ya mama ikisema ‘Haya laleni sisi tunaenda dansini’. Mara ya kwanza kuona watu wakicheza dansi ilikuwa nyakati hizohizo. Pale ulipo sasa Uwanja wa Samora , kulikuwa na shule ya pili…
