WAPIGA MAGITAA YA SOLO WALIWEKA NEMBO ZA BENDI
Katika muziki wa dansi wa Tanzania kati ya mwaka 1960 na mpaka 1990, bendi zilikuwa na utaratibu wa kutumia magitaa matatu au manne. Kulikuwa na gitaa lililoongoza ambalo lilijulikana kama gitaa la solo, kisha kukaweko gitaa lililosindikiza lililoitwa gitaa la ridhim na kukaweko na gitaa zito lililojulikana kama gitaa la bezi na mwisho kulikuwa na…
